Sibuka FM

Vifo vitokanavyo na Uzazi vyapungua Wilayani Maswa

19 April 2021, 5:09 pm

Vifo  vitokanavyo  na  Uzazi  wilayani  Maswa  mkoani  Simiyu vimepungua  kutoka vifo  12  kwa  mwaka  2018  hadi  kufikia  vifo  3  kwa  mwaka  2020.

Takwimu  hizo  zimetolewa  na  Mratibu  wa  Huduma  ya  Mama  ya  mtoto  kutoka  Hospitali  ya  wilaya ya  Maswa  Angella  Ngaiza  wakati  akitoa  Elimu  ya  Afya  ya   Uzazi  kupitia  Radio  Sibuka  fm.

       

Sauti ya Mratibu wa Huduma ya mama na mtoto Angella Ngaiza

Bi   Ngaiza   amesema  kuwa  kupungua  kwa  vifo  hivyo  kumetokana  na  Mikakati  ya  Halmashauri   ya  wilaya,   Wadau   wa  Afya  na  kituo  cha  Radio Sibuka   kwa  kusaidia kutoa  Elimu ya  Afya  ya Uzazi  na  kuwafika  watu  wengi  zaidi na  kuongeza kuwa  vifo  hivyo  vinapoteza   nguvu  kazi  ya  Taifa.

       

Sauti ya Angela  Ngaiza

Aidha  Mratibu  huyo wa  Huduma  ya  Mama  na Mtoto  amesema  kuwa  Ushiriki  wa  Mwanaume  katika  Huduma ya  Afya  ya  mama  kuna  nafasi  kubwa  ya  Mama  kujifungua   Salama    Hivyo  ni vyema  Jamii  ikaondoa  mazoea  na  dhana   ya  kuwa wazazi  wa  zamani  walikuwa  wanajifungulia  nyumbani  bila  madhara  yoyote   kwani  kwa  sasa  mambo  yamebadilika.

Sauti ya Angela  Ngaiza
Mratibu wa Huduma ya mama na mtoto Angella Ngaiza