Wananchi Waaswa kula mlo wenye Makundi 5 ya Chakula.
15 February 2023, 3:08 pm
Wananchi Wilayani Maswa wameaswa kula chakula chenye Makundi Matano ya chakula Bora ili Kuimarisha Afya.
Hayo yamesemwa mapema hii leo na Afisa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Ndugu Abel Gyunda Wakati akitoa Elimu ya Masuala ya Lishe na ulaji wa chakula kwa kuzingatia makundi Matano kupitia Radio Sibuka fm.
Ndugu Gyunda amesema kuwa Mara nyingi watu wanakula aina moja au mawili na kuona ndio wamekula mlo kamili kitu ambacho siyo Sahihi..
” Mtu akila Ugali na Samaki anajua amekula mlo kamili wakati kuna makundi mengine ya chakula hayajahusika kuufanya mlo uwe Kamili kwa Afya..
Aidha Afisa Lishe amesema kuwa Maeneo yetu ya Simiyu Wananchi Wanalima sana Mazao ya Chakula na kuzalisha kwa Wingi lakini bado kuna hali ya Udumavu kwa Watoto.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takimu Mkoa wa Simiyu unashika Nafasi ya Saba katika Mikoa 12 inayoongoza kwa hali ya Udumavu kwa Watoto ikiwa na Asilimia 33.2%.