Takukuru yatambulisha Programu ya ”TAKUKURU-Rafiki’
30 January 2023, 4:29 pm
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Wilayani Maswa Imezidua na Kutambalisha kwa Madiwani Programu ya TAKUKURU- RAFIKI ikiwa na lengo la Kuongeza Ushiriki wa Kila Mwananchi na Wadau mbalimbali katika kukabiliana na tatizo la Rushwa katika Utoaji wa Huduma kwa Jamii na Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Akitambulisha Programu hiyo kwenye Kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Afisa Takukuru Wilayani hapo Bi Alpha Malisa amesema kuwa Proramu ya TAKUKURU -Rafiki itasaidia kukuza Ustawi na Utawala Bora kwa Kuzuia vitendo vya Rushwa visitokee..
Aidha Bi Malisa ameongeza kuwa Programu hii itasaidia kutekeleza Miradi ya maendeleo kwa Ufasaha kwani kutakuwa hamna mianya ya Rushwa inayorudisha nyuma Maendeleo na Mirdi kujengwa chini ya Viwango.
Mohamedi Dase Diwani wa Kata ya Seng’wa na Silvanus Mipawa Diwani wa Kata ya Buchambi Wilayani Maswa Wamesema kuwa huduma hii itasaidia kuwaweka wananchi karibu na kuwa Huru kutoa taarifa za Mianya ya Rushwa tofauti na hapo zamani Takukuru ilikuwa mbali na Wananchi hivyo kushindwa kutoa Ushirikiano.
Bi Malisa amesema Programu hii inatekelezwa kwa Nchi nzima ambapo kauli Mbiu yake ni Kuzuia Rushwa ni Jukumu langu na lako, Tutimize wajibu wetu..
Hapa chini ni Matukio ya Picha katika Baraza la Madiwani wakati wa Utambulisho wa Programu ya TAKUKURU- Rafiki