Milioni 160 kununua Dira za maji Maswa
31 March 2021, 12:55 pm
Zaidi ya shilingi Milioni 160 zimetolewa na serikali ya jamhuri ya muunga no wa tanzania kwa ajili ya ununuzi wa dira za maji ili kila mtu anayetumia alipe kwa kadri ya matumizi yake.
Hayo yamesema na mkuu wa wilaya ya Maswa Mh, Aswege Kaminyoge wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwakwe na kusema kuwa ufungwaji wa dira hizo zitaongeza ukusanyaji wa mapato yatakayosaidia uendeshaji wa Mamlaka hiyo…
Mh. Kaminyoge amesema kuwa pamoja na Serikali kutumia gharama kubwa katika ujenzi wa mradi wa chujio wananchi wanapaswa kulinda bwawa hilo ambalo ndio chanzo kikuu cha maji kwa mji wa Maswa.
Mwenyekiti wa bodi ya maji Maswa Paulina Ntagaye amesema kuwa mradi wa chujio la maji umekamilika kwa asilimia mia moja hivyo kwa sasa wananchi wa maswa wanatapa Maji safi na Salama na kuongeza kuwa wananchi wanatakiwa kuwafichua wanaohujumu miundo mbinu ya Maji.
Aidha kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya maji maswa -MAUWASA Mhandisi Nandi Mathias amesema kuwa kukamilika kwa Mradi kumesaidia kumtua mama ndoo kichwa pamoja na na kuondokana na changamoto ya maji machafu yaliyokuwa yanatoka hapo awali..
Naye diwani wa kata ya Zanzui Jeremia Shigala Mange pamoja na baadhi ya wananchi wameishukuru serikali kwa kutoa fedha za ujenzi wa mradi huo wa chujio ambao umewezesha wananchi Kupata huduma ya maji safi na Salama.
Kauli mbiu ya wiki ya Maji kwa mwaka huu 2021 ni … “”thamani ya Maji kwa Uhai na Maendeleo”