WENYEVITI WA VITONGOJI ZAIDI YA 40 WILAYANI MASWA WAGOMEA POSHO YA ELFU TANO KATIKA ZOEZI LA UANDIKISHAJI WA ANUANI ZA MAKAZI NA POSTIKODI.
21 March 2022, 8:18 pm
Wenyeviti wa vitongoji zaidi ya Arobaini wanaounda Mamlaka ya Mji mdogo Maswa wamegoma kushiriki zoezi la Uandikishaji wa anuani za Makazi kutokana na Kupunjwa Posho katika Zoezi la Uandikishaji wa Anuani za Makazi hivyo kupelekea kuomba Mwongozo wa Halmashauri kuhusu Ulipwaji wa Posho hizo.
Wenyeviti hao wakiwa wamekusanyika kwenye Ukumbi wa Mamlaka ya Mji mdogo wamedai kuwa zoezi hilo ni gumu na linahitaji Umakini hivyo haifai kulipwa shilingi Elfu Tano kwa siku na kama Halmashauri haina bajeti ni vyema wakaacha kushiriki katika Zoezi hilo.
Wenyeviti hao wamesema kuwa mara nyingi serikali imekuwa ikiwasahau na kutojali Masilahi yao licha ya wao kuhusika na zoezi hilo moja kwa moja kwani wao ndio wanazitambua kaya na Mipaka ya maeneo yao.
Aidha wamesema kuwa awali waliambiwa kuorodhesha majina ya Barabara kwenye vitongoji na Mitaa yao na kuyawasilisha Halmashauri kasha kurudishiwa Nakala ili ziwasaidie kujua barabara zilizopitishwa na Halmashauri huku wakidai Zoezi la kupata vijana watakaofanya kazi za Kuweka Anuani za Makazi liligubikwa na Urasimu.
Baada ya mgomo huo na malalamiko ya Kupunjwa Posho, Mratibu wa zoezi hilo la Anuani za Mkazi wilayani Maswa Ndugu Edwini Bairu akawasilisha Mwongozo wa Halmashauri ya Maswa kuhusu utaratibu wa Ulipwaji wa Posho za wenyeviti wa vitongoji na Mitaa na kuahidi kuwaongezea elfu Tano ili ifike Elfu kumi ili wakafanye Zoezi hilo Muhimu.
Hapa chini ni baadhi ya wenyeviti wa vitongoji wanaunda Mamlaka ya Mji mdogo Maswa.