Serikali Mkoani Simiyu kujenga Mabweni ya wanafunzi wa kike ili Kunusuru Mimba za Utototni..
25 February 2022, 5:50 pm
Serikali Mkoani Simiyu inatarajia kutumia zaidi ya shilingi Bilion 6 kujenga mabweni kwa ajili ya kuwanusuru na Mimba za Utotoni watoto wanaotoka kwenye kaya masikini wanaosoma Shule za Sekondari Mkoani hapa.
Akizungumza na wakazi wa Wilayani Maswa Mkoani Simiyu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Madeko Mkuu wa Mkoa Mh, David Zacharia Kafulila amesema kuwa ujenzi huo wa mabweni utaanza kutekelezwa kwa mwaka wa fedha 2022/2023..
Giladius Michael Lwezaura ni Mwalimu Mkuu shule ya Sekondari Nyalikungu iliyopo wilayani hapa amesema watoto wa kike wamekuwa wakikutana na changamoto kubwa kutokana na kukosekana kwa Mabweni ya wanafunzi wa kike..
Aidha Mwalimu Eliud Kabengo amesema kuwa mara nyingi wanafunzi wa kike wanaporudi nyumbani baada ya Masomo ya Darasani wamekuwa wakifanyishwa kazi za majumbani hali inayopelekea kukosa Muda wa kujisomea..
Naye Monica Malale Gogadi kutoka shule ya Sekondari Nyalikungu ameiomba serikali ya Rais Samia Suluhu Hasani kuona Umuhimu wa kujenga mabweni kwa watoto wa kike ili kuondoa changamoto zinazowakabili na kuongeza Ufaulu katika Masomo yao.
Nao baadhi ya wananchi wamepongeza mpango huo wa Serikali wa kujenga Mabweni kwa ajili ya watoto wa kike kwani itasaidia tatizo la Mimba za Utotoni ambazo zimekuwa zikitatiza ndoto zao.