Taasisi ya TWAWEZA yatoa Mafunzo Kwa Waraghabishi Wilayani Maswa.
22 February 2022, 6:02 pm
Jumla ya Waraghabishi Thelathini na sita (36) kutoka kata 18 za wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu wamepewa Mafunzo ya kuwawezesha kuibua changamoto na Vipaumbele vya Maendeleo kwenye maeneo ya vijiji vyao.
Akizungumza na Sibuka Fm Meneja Programu kutoka Shrika la Kawie Social Development Foundation (KASODEFO) Marius Isavika amesema kuwa lengo la kukutanisha Waraghabishi hao ni kupitia Changamoto zilizoibuliwa katika kipindi cha Utafiti Shirikishi kwa Wananchi..
Isavika amesema kuwa wanalenga kufika kata zote za wilaya ya Maswa ambapo ndipo Mradi huo unatekelezwa ili waanchi wawe na Uwezo wa Uibua na Kubaina Changamoto zinazowakabili na kuzitafutia Ufumbuzi..
Rukia Masanyika ni mwezeshaji kutoka Taasisi ya TWAWEZA amesema kuwa Uraghabishi ni Dhana ambayo inalenga kusaidia wana Jamii kuibua hoja zao wenyewe ..
Nao baadhi ya Wadau na Washriki wa Mafunzo hayo wamesema kuwa wamejifunza mbinu mbalimbali za kushirikisha Jamii katika kuimbua Masuala mbali ya maendeleo..
Hapa chini ni Baadhi ya Picha za Washiriki wakiwa katika Mafunzo ya Uraghabishi.