WILAYA YA MASWA YATAJWA KUONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KWA MKOA WA SIMIYU..
29 December 2021, 11:50 am
Imeelezwa kuwa wilaya ya maswa inaongoza kwa maambukizi ya Virusi ya Ukimwi (VVU) Ikifuatiwa na Wilaya Busega katika mkoa wa Simiyu.
Hayo yameelezwa na Mratibbu wa Ukimwi mkoa wa Simiyu Dr Hamis Kulemba wakati akizungumza na Radio Sibuka.
Dr Kulemba amesema kuwa vichocheo vikubwa vinavyopelekea maambukizi kuongezeka ni tabia ya kuwa Wenza wengi, Wadada kujihusisha na Biashara za Ngono na pamoja na migodi ya madini, kambi za ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR)..
Aidha Dr Kulemba ametoa wito kwa jamii ya mkoa wa simiyu kila mmoja kutambua VVU na Ukimwi Upo na unaua hivyo ni vyema kupima na kutambua hali ya Afya zetu..
Amesema kuwa kuanza kiliniki mapema kwa mama wajawazito kutasaidia kupunguza watoto kuzaliwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi hivyo kupeekea kupunguza vifo kwa watoto wanaozaliwa na VVU…
……..Mwisho……