hakielimu yatoa mafunzo na vyerehani kwa watoto wa kike ili kushona taulo za kike
13 October 2021, 2:30 pm
Katika kukabiliana na changamoto za watoto wa kike kutohudhuria kikamilifu masomo yao hakielimu kupitia mradi wa The Girls Retention and Transition Initiative (G.R.T.I ) imetoa vyerehani na mafunzo kwa wanafunzi kutegeneza taulo za kike ili waweze kujihifadhi kipindi cha hedhi .
Hayo yamesemwa na walezi wa vinara kupitia mradi wa G.R.T. I ambapo wameongeza kuwa kabla ya mafunzo hayo baadhi ya watoto wa kike hususan wanafunzi walikuwa wanatumia vitu ambavyo ni hatari kwa afya zao.
Janeth Jackson ni afisa ustawi wa jamii kutoka halmashauri ya mji wa Bariadi amesema kuwa vitendo vya ukatili vinatolewa taarifa zikiwa zimecheleweshwa huku afisa maendeleo ya jamii kutoka halmashauri ya mji wa Bariadi Hollo Ngeme akiongea kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo amewapongeza haki elimu kwa kutoa mafunzo ya namna ya kutengeneza taulo za kike.
Nao baadhi ya wanafunzi wameomba jamii hususan wazazi na walezi wawe wanapewa elimu dhidi ya kupinga vitendo vya ukatilii wa kijinsia huku wakiwaomba watoto wa kike wasirubuniwe ili na wao wafikie malengo yao.
Maadhimisho hayo yamefanyika kwa mara ya kwanza mkoani hapa yakiwa na kauli mbiu isemayo “kizazi cha kidijitali ,kizazi chetu” huku yakienda sambamba na maigizo na burudani kutoka kwa wanafunzi wa vinara kutoka baadhi ya shule za msingi na sekondari zilizopo mkoani hapa.