RC Kafulila; Bei ya Pamba yavunja rekodi Msimu wa 2020/2021.
17 September 2021, 4:56 pm
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh, Davidi Zacharia Kafulila amesema kuwa bei ya Pamba kwa mwaka huu wa 2021 imevunja rekodi ya zaidi ya miaka Ishirini iliyopita kutokana na Usimamizi Bora wa mifumo ya ununuzi wa zao la Pamba..
Mh Kafulila amesema kuwa kupanda kwa bei ya Pamba imetokana na maelekezo ya Rais wa awamu ya sita Mh Samia Suruhu Hasani kwamba hakuna ujanja ujanja katika bei kwakuwa wakulima wengi hawajui bei ya Pamba katika soko la Dunia.
Aidha mkoa wa Simiyu umepokea nyingi kwa ajili ya shughuli za maendeleo ambapo amewataka viongozi wenzake kusimamia fedha hizo ili zilete tija kwa wananchi .
Mh Kafulila akiwa katika ziara yake wilayani Meatu amefanya mikutano ya hadhara katika maeneo mbali mbali na kusikiliza kero za wananchi ikiwa ni utaratibu aliojiwekea huku hoja zikiibuka katika sekta ya Pamba, Afya na Elimu.