Wenyeviti wa vitongoji Mamlaka ya Mji Maswa waapishwa, tayari kwa majukumu
28 November 2024, 7:34 pm
Niwapongeze kwa Ushindi mliopata hivyo saivi ni Wenyeviti wa Vitongoji rasmi, Nendeni mkawatumikie Wananchi kwani wanachangamoto nyingi katika maeneo yao – DED Maswa Maisha Mtipa https://maswadc.go.tz/
Jumla ya Wenyeviti wa Vitongoji 40 kutoka kata Nne zinazounda Mamlaka ya Mji Mdogo Katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu Wameapishwa rasmi kwa ajili ya kwenda kuwatumikia Wananchi baada ya Kumalizika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Nov, 27, 2024.
Akiwaapisha Wenyeviti hao, Hakimu Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Maswa Mhe Enos Sylvester Misana amesema kuwa ni Vizuri wakatunza na kutekeleza Viapo vyao kwani nafasi walizo nazo ni kubwa na Muhimu kwa Maslahi ya Wananchi.
Akitoa Nasaha kwa Wajumbe hao wanaunda Baraza la Mamlaka ya Mji mdogo Maswa , Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndugu Maisha Mtipa amesema kuwa Wananchi wanachangamoto nyingi katika Maeneo yao hivyo Wakasaidie kutatua changamoto hizo au kuzifikisha ngazi za juu kwa ajili ya utatuzi zaidi
Mtipa ameongeza kuwa baada ya kuapishwa sasa wakafanye kazi za Kuwahudumia Wananchi Pamoja na Usimamizi wa Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa katika ngazi za Vijiji na Vitongoji na kusimamia Ukusanyaji wa Mapato ili Mipango yote ya Maendeleo iweze kutekelezeka kwa Wakati.
Sibuka FM imezungumza na baadhi ya Wenyeviti wa Vitongoji walioapa na kusema wataenda kutatua changamoto za Wananchi na kutekeleza Vipao mbele vyote walivyoahidi wakati wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa