Wananchi Maswa wapongeza zoezi la upigaji kura uchaguzi serikali za mitaa
27 November 2024, 4:03 pm
Wananchi Wilayani Maswa Mkoani Simiyu Wameipongeza Serikali kwa Mandalizi Mazuri ya zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika leo Nov, 17, 2024
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kupiga kura wamesema kuwa wananchi wamehamasika kupiga kura kwa Wingi ili kuchagua Viongozi katika Maeneo yao kulingana na Mazingira rafiki ya kupigia kura yaliyowekwa na Serikali.
Maisha Mtipa ni Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Maswa amesema kuwa zoezi linaenda Vizuri hajapokea changamoto yoyote katika Upigaji wa Kura na Vituo vimefunguliwa kwa Wakati licha ya kuwepo kwa changamoto ya Mvua.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais , Mipango na Uwekezaji Mhe Stanslaus Nyongo amesema kuwa Zoezi limekuwa na Utulivu wa hali ya juu huku akitoa rai kwa wananchi kujitokeza kupiga kura na kurudi majumbani ili kusubiria Matokeo
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe, Aswege Kaminyoge ameshiriki katika kupiga kura katika Kitongoji cha Mwantonja kata ya Nyalikungu Wilayani hapa na kusema kuwa Zaidi ya Wananchi Laki moja na Hamsini na Tano Elfu (155,000) walijiandikisha huku kukiwa na Jumla ya Vituo Mia tano na kumi (510) vya kupigia kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.