Jaccafo yafanya maadhimisho ya watu wenye ulemavu Maswa
6 December 2023, 8:27 pm
Jamii wilayani Maswa imeaswa kuwafichua watoto wenye ulemavu waliofungiwa majumbani ili waweze kuzifikia ndoto zao kielimu, kiuchumi na kijamii.
Na Alex Sayi
Shiriki lisilo la kiserikali la Juniors and Child Care Foundation (JACCAFO) limefanya maadhimisho ya siku ya walemavu Duniani kwa mara ya kwanza Wilayani Maswa Mkoani Simiyu, lengo ikiwa ni kuihamasisha jamii ya watu wenye ulemavu kushiriki shughuli za kijami.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Shirika hilo Joseph Ngeleja Jidayi kwenye maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu Duniani yaliyofanyika Desemba 04/mwaka huu Shule ya Msingi Binza Wilayani Maswa Mkoani hapa.
Awali kabla ya maadhimisho hayo maafisa wa Shirika hilo walitembelea baadhi ya Wodi kwenye Hospitali ya Wilaya Maswa nakutoa misada mbalimbali kwa watoto,kwa wajawazito nakwa wazazi waliojifungua watoto njiti.
Dkt,Hagai Timothy Mganga mfawidhi Hospitali ya Wilaya Maswa Mkoani hapo aliushukuru uongozi wa (JACCAFO)kwa msaada walioutoa nakuuomba uongozi wa Shirika hilo kuielimisha jamii hasa kinamama wajawazito kuona umuhimu wa kuhudhuria Clinik
Kwa upande wake mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo Saguda Sayayi Afisa Tarafa Tarafa ya Sengerema Wilayani hapa akizungumza kwa niaba ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya amesema kuwa watoto wenye ulemavu wana haki sawa na watoto wengine.
Akisoma taarifa fupi ya kitengo cha watoto wenye mahitaji maalumu Mwl,Christopher Makongo amesema kuwa kitengo kilianzishwa mwaka (2006)kikiwa na wanafunzi wanne hadi sasa kitengo hicho kinajumla ya watoto kumi na tano
Gange Bukwimba mkazi wa kijiji kwa Igwata Kata ya Nyabubinza Wilayani hapa ametoa shukrani zake kwa Shirika hilo kwakumsaidia mwanae kupata msaada wa kiti mwendo huku akizungumzia adha alizokuwa akizipata mwanae kabla ya kupata msaada huo.