CCWT kuanza usajili wafugaji kwa njia ya kielektronik
19 November 2023, 5:37 pm
Chama Cha Wafugaji Taifa (CCWT) ziarani nchi nzima kuhamasisha wafugaji kujisajili kwa njia ya kielektronik ili wafugaji hao wawe na chombo cha kuwaunganisha na kutatua matatizo yao.
Na Alex Sayi.
Chama Cha Wafugaji Taifa kimeendelea na ziara nchi nzima kwa lengo la kuwahamasisha wafugaji na Wakulima kujiunga na chama hicho kwa kufanya usajiri kwa njia ya Kieletronic
Kusundwa Wamalwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Wafugaji Taifa amesema kuwa (CCWT) kinaendelea na kampeni nchi nzima ya kuhakikisha wafugaji na wakulima wanajisajili ili waweze kutambuliwa na serikali na kuwa na tqkwimu sahihi za mifugo.
Wamalwa akizungumzia baadhi ya changamoto zinazowakabili wafugaji amesema kuwa kilimo kimekuwa chanzo kikubwa cha uharibifu wa mazingira licha ya watalaam kudai kuwa ng’ombe zinachangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira.
Nao baadhi ya Wafugaji Wilayani Maswa Mkoani Simiyu wamezungumzia baadhi ya changamoto zinazowakabili Wafugaji hao,Ngasa Sanyangi amesema kuwa kumekuwa na dhana potofu kuhusiana na Chama hicho cha Wafugaji.
Akitolea ufafanuzi wa Suala hilo Sylivery Buyaga Katibu Masidizi (CCWT) Kanda ya Nyanza na Afisa Idara ya Sheria (CCWT)Makao Makuu Dodoma alisema kuwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama hicho kinasema kuwa (CCWT)haijihusishi na masuala yoyote ya kisiasa.
Dkt,Christopher Nzela Mratibu na Katibu wa Migogoro(CCWT)amewaomba wafugaji na wakulima wajiunge na Chama hicho ili Chama kiwe na nguvu ya kuwasemae Wafugaji hao pindi migogoro inapojitokeza