Maswa: RC aagiza hoja zote za CAG zifungwe
22 June 2023, 7:13 pm
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda ameuagiza
uongozi wa wilaya ya Maswa kuhakikisha wanafunga hoja zote
za Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) zilizotolewa
baada ya kufanya ukaguzi wa fedha kwa mwaka wa fedha
2021/2022.
Dkt Nawanda ametoa maagizo hayo wilayani Maswa wakati wa
kikao cha Baraza Maalum la kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti
wa Hesabu za Serikali (CAG) huku akitoa siku kumi (10) kwa
halmashauri ya wilaya ya Maswa kulipa madeni ya fedha za
wastaafu kwenye mifuko ya jamii ili waweze kupata mafao yao..
Sauti ya RC Simiyu Dkt Yahaya Nawada
Aidha Dkt Nawanda amesema kuwa Halmashauri ya Maswa imekuwa ya Mwisho katika Ukusanyaji wa Mapato ikilinganishwa na Halmashauri zingine za Mkoa wa Simiyu huku akiwataka Wakuu wa Idara kubuni vyanzo vya Mapato vitakavyosaidia kuongeza ukusanyaji wa Mapato na kufikia Malengo iliyojipangia..
Sauti ya RC Simiyu Dkt Yahaya Nawad
Akiwasilisha taarifa ya ukaguzi wa hoja za CAG kwa mwaka wa
fedha 2021/2022, mkaguzi wa nje wa hesabu za serikali za mitaa
mkoa wa Simiyu Gwamaka Mwakyosi amesema kuwa halmashauri
ya wilaya ya Maswa imepata hati safi hivyo waendelee kufuata
taratibu zote za uendeshaji wa halmashauri ili kuepuka kupata hati
chafu..
Sauti ya Gwamaka Mwakyosi
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Maswa Mhe, Paul Maige
amesema kuwa watazingatia ushauri wote uliotolewa na ofisi ya
Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali ili kuhakikisha
wanaondoa hoja zote na kutoruhusu hoja mpya ambazo zinaweza
kuwachafulia hata.
Sauti ya mwenyekiti wa Halmashauri Paul Maige
Aswege Kaminyoge ni mkuu wa wilaya ya Maswa amesema kuwa
anajivunia kufanya kazi na madiwani kwani amekuwa akipata
Ushirikiano wa kutosha katika kuwaletea maendeleo wananchi wa
Maswa.
Sauti ya DC Maswa Aswege Kaminyoge
Akitoa neno la shukrani kwa niaba ya madiwani wenzake, diwani
wa kata ya Zanzui hapa Maswa Mhe. Jeremia Shigala maarufu kwa
jina la Makondeko amesema kuwa anawashukuru viongozi
waliotoa mapendekezo ya namna ya kuboresha usimamizi na
ukusanyaji wa mapato.
Sauti ya Diwani kata ya Zanzui Jeremia Shigala