Sibuka FM

Anamringi: Zimamoto washirikishwe kabla ya ujenzi wa majengo kuanza

14 January 2026, 8:04 pm

Kwenye picha ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Anamringi Macha akizungumza jambo na wananchi (hawapo pichani). Picha kutoka maktaba ya Sibuka Fm

Tunahitaji kumaliza au kupunguza majanga ya moto kuunguza nyumba elimu pekee tu haitoshi lazima sasa tuweke mashariti magumu kidogo lakini kwa manufaa ya badae tunaweza kujenga majengo bila ushauri wa jeshi la zimamoto na uokoaji ni muda sasa wa kubadilika tuwasikilize kwa zimamoto kabla ya kuanza ujenzi.”

Na,Daniel Manyanga 

Mkuu wa mkoa wa Simiyu ,Anamringi Macha amezitaka taasisi zote za serikali mkoani hapo kulishirikisha jeshi la zimamoto na uokoaji katika miradi ya ujenzi wa majengo mablimbali, kabla ya kuanza utekelezaji wa miradi hiyo ili waweze kupata ushauri juu ya namna bora za kujikinga na kuyaepusha majengo hao dhidi ya majanga ya moto.

Anamringi Macha ametoa agizo hilo wakati akizungumza katika hafla fupi iliyoandaliwa na jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Simiyu kwa ajili ya kuwaaga maaskari wastaafu na kuwakaribisha maaskari wapya wa jeshi hilo iliyofanyika mjini Bariadi, ambapo amesema ni muhimu jeshi hilo likashirikishwa kabla ya kuanza utekelezaji wa miradi ya ujenzi. 

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Simiyu, Anamringi Macha akizitaka taasisi za kiserikali kushirikisha jeshi la zimamoto na uokoaji kabla ya kuanza ujenzi
Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Simiyu, Mrakibu Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Faustine Mtitu Picha kutoka maktaba ya Sibuka Fm

Awali akizungumza katika hafla hiyo, kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu, mrakibu msaidizi wa jeshi la zimamoto na uokoaji Faustin Mtitu amewataka wananchi mkoani hapo kutoa taarifa kwa haraka wanapokumbwa na matukio ya moto.

Sauti ya kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu, mrakibu msaidizi wa jeshi zimamoto na uokoaji, Faustine Mtitu

John Sabu na Nassoro Rashid ni baadhi ya wakazi wa Simiyu walioshiriki hafla hiyo wakaeleza namna ambavyo ushirikiano uliopo baina ya jeshi la zimamoto na wananchi mkoani Simiyu unasaidia kupunguza athari mbalimbali zitokanazo na moto au matukio mengine yanayohitaji maokozi.

Sauti ya wananchi baadhi walihudhuria hafla hiyo