Sibuka FM

DC Maswa ataka uzalendo kwa watumishi wa umma

19 November 2025, 11:00 am

Pichani ni muonekano wa nje wa jengo jipya la makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Maswa lililopo jengwa katika kijiji cha Nh’ami kata ya Nyalikungu na kugharimu zaidi ya billion tatu mpaka sasa Picha kutoka maktaba ya Sibuka Fm

Kwa nini kila kukicha tunaimba uzalendo uzalendo kwa watumishi wa umma nini kimekosekana mpaka tunaanza kukumbushana kwani wao hawajui maana ya neno la uzalendo au wao wanalijuwa kulisoma tu lakini kwenye vitendo ni hakuna ukiona hivyo juwa kuna kitu hakipo sawa”.

 Na,Daniel Manyanga 

Mkuu wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Dkt.Vicent Naano Anney amewataka watumishi wa umma na wananchi kuwa wazalendo wa taifa hili ili waweze kuacha hadithi nzuri itakayoweza kukumbukwa na vizazi vingi pale watakapokuwa hawapo kwenye nafasi za uongozi na hapa duniani.

Pichani ni mkuu wa wilaya ya Maswa, Dkt.Vicent Naano Anney aliyesimama mwenye suti nyeusi akiwa na kipaza sauti akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Maswa Picha kwa hisani ya Samwel Mwanga

Dkt.Vicent Naano Anney akizungumza kwenye hafla ya ufunguzi wa jengo jipya la makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Maswa lililopo katika kijiji cha Nh’ami kata ya Nyalikungu ufunguzi uliohudhuriwa na watumishi wa umma,viongozi wa dini,kamati ya ulinzi na usalama wilaya ,viongozi wa kimila na wananchi wa maeneo hayo jengo lililogharimu kiasi cha fedha billion tatu na milioni miatatu mpaka hivi sasa huku ukamilishaji ukiwa bado unaendelea.

Sauti ya Dkt.Vicent Naano Anney mkuu wa wilaya ya Maswa akiomba uzalendo kwanza kwa watumishi wa halmashauri hiyo

Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ya Maswa,Dkt.Vicent Naano Anney ameiomba hadhara hiyo iliyohudhuria ufunguzi wa jengo hilo kuipenda na kuijenga  nchi hii maana hakuna nchi nyingine kama Tanzania.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Maswa, Dkt.Vicent Naano Anney akizungumza na hadhara na kuiomba kuipenda na kuijenga nchi hii