Sibuka FM
Sibuka FM
18 November 2025, 12:25 pm

“Uzuri wa jengo kipya la makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Maswa ukatoe utendaji mzuri kwa watumishi wa umma katika kuwahudumia wananchi ili kutoa tafsiri sahihi ya uzuri wa jengo na kuleta tabasamu kwa wakazi wa wilaya”.
Na,Daniel Manyanga
Mkuu wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, Dkt.Vicent Naano Anney amewaomba watumishi wa umma kufanya kazi kwa bidii katika kuwahudumia wananchi wilayani hapo pamoja na kutunza jengo jipya la makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Maswa lililopo kijiji cha Nh’ami kata ya Nyalikungu ili liweze kudumu.

Dkt.Anney ametoa rai hiyo wakati akizungumza na watumishi hao wa halmashauri ya wilaya hiyo walipokuwa wanahamia kwenye jengo hilo hafla iliyohudhuriwa na viongozi kamati ya ulinzi na usalama wilaya,watumishi wa umma,viongozi wa chama ,viongozi wa dini na kimila.
Mkuu huyo wa wilaya ameishauri halmashauri hiyo kutangaza uuzaji wa viwanja vilivyopo karibu na jengo hilo ili kufungua uchumi katika maeneo hayo huku viongozi wa dini wakiombwa kuhubiri amani na mshikamano.
Kwa upande wake afisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya Maswa, Julius Ikongora amesema kuwa utekelezaji wa mradi wa jengo hilo ulianza mwaka 2023 na unategemea kumalizika mwishoni mwa mwaka huu huku zaidi ya billion tatu zikitumika katika ujenzi wa jengo hilo.