Sibuka FM
Sibuka FM
28 October 2025, 11:55 am

Jiepusheni na magroup songozi ya mitandaoni ili msije mkakosea na kutuma huko taarifa pia Jiepusheni na ushabiki wa vyama vya Siasa msije mkaleta tahaluki kwani nyie mnafanya kazi kwa niaba ya Tume huru ya Taifaya Uchaguzi ”Julius Ikongora John “
Wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura katika Jimbo la Maswa mashariki na Jimbo la Maswa magharibi wameaswa kutunza siri kama walivyoapa kwa mjibu wa sheria na kanuni za Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi hivyo wajiepushe na magroup songozi ya mitandao ya kijamii ili kuepuka kukosea na kutuma taarifa kwenye magroup hayo.
Hayo yamesemwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Maswa mashariki na Jimbo la Maswa Maghariki Ndugu Julius Ikongora John wakati wa kufunga mafunzo kwa wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura
Aidha Ndugu Julius Ikongora amewataka wasimamizi hao kuhakikisha wanazingatia muda wa kufungua vituo na kufunga vituo, kufanya kazi kwa Weledi na Uzalendo, kufanya kazi kwa ushirikiano na kuzingatia miongozo na kanuni za Uchaguzi.
Ameongeza kuwa wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa vituo wanapaswa kuwa na Lugha nzuri kwa wapiga kura na kutoa vipaumbele kwa makundi maalumu ya Watu wenye Ulemavu, wazee, wajawazito na akina mama wanaonyonyesha huku wakijiepusha na ushabiki wa vyama vya siasa.
Baadhi ya wasimamizi wa vituo vya kupigia kura wamezungumza na sibuka Fm na kueleza watakavyoenda kuzingatia maelekezo yote waliyopewa na Tume ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa haki na usalama, wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura kwani ni haki yao ya msingi – “ Kura yako haki yako , Jitokeze kupiga kura”

