Sibuka FM
Sibuka FM
25 October 2025, 3:16 pm

Makarani waongozaji wapiga Kura katika Jimbo la Maswa Mashariki na Jimbo la Maswa Magharibi wameaswa kuzingatia Kanuni, Miongozo na Sheria za Uchaguzi zilizotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi ili kuepuka migogoro isiyokuwa ya lazima
Nasaha hizo zimetolewa na Msimizi wa Uchaguzi Jimbo la Maswa Mashariki na Maswa Magharibi Ndugu Julius Ikongora John leo Oktoba 25, 2025 wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya siku moja kwa Makarani waongozaji yaliyofanyika katika Ukumbi wa Msechu Wilayani hapa
Ndugu Ikongora ameongeza kuwa uteuzi wa Makarani hao umezingatia kifungu cha 76 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Namba 1 wa Mwaka 2025 , hivyo wana wajibu wa kutekeleza majukumu ya Uchaguzi kwa niaba ya Tume

Awali akitoa ufafanuzi kwa Makarani waongozaji juu ya Sheria za Uchaguzi , Msimamizi msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Wilayani ndugu Masanja Kengese amewataka Makarani hao kuviishi viapo vyao wakati wote wa utekelezaji wa shughuli za Uchaguzi.
Nao baadhi ya Makarani waongozaji wa Uchaguzi wamezungumzia namna walivyojiandaa kutekeleza majukumu yao pamoja na kutoa vipaumbele kwa makundi maalumu ikiwemo wazee, watu wenye ulemavu na akina mama wajawazito na wanaonyonyesha

