Sibuka FM

Dkt Lugomela arejesha fomu ya Ubunge, ataja vipaumbele vyake

27 August 2025, 11:23 pm

Picha (mwenye miwani mbele ) Dkt George Lugomela akirejesha fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi ya Ubunge kupitia ccm Jimbo la Maswa mashariki. Na Nicholaus Machunda

Maswa imekuwa nyuma kimaendeleo kuna mambo hayako sawa ikiwemo suala la changamoto ya zao la pamba ambalo ndio zao kuu la biashara kwa mkoa wetu wa Simiyu lakini inashangaza Bei inaendelea Kushuka kila msimu na wakulima kukopwa pamba yao hivyo nitaenda kuboresha changamoto hiyo ” Dkt George Lugomela “

Mgombe  Ubunge  Jimbo  la  Maswa  Mashariki  kupitia  chama cha  Mapinduzi ccm    Dkt  George Lugomela amerejesha  fomu  ya  uteuzi  wa kugombea nafasi hiyo  huku  akitaja  vipaumbele  vyake  ni  maji, elimu,  afya   pamoja  kushughulikia  changamoto za zao  la  Pamba  ili  lilete  tija  kwa  wakulima.

sauti ya George Lugomela mgombea ubunge Maswa mashariki- ccm

Dkt  Lugomela  amesema  kuwa  anawashukuru  wote  waliompigia  kura na wale ambao hawakumpigia  katika  mchakato wa  kura  za  maoni  kwani alikuwa  na  ndoto  ya  muda  mrefu  ya  kuwatumikia  wana  Maswa  kupitia  nafasi  ya  Ubunge  na  kuahidi  kuwa  mbunge wa  watu  wote.

sauti ya George Lugomela mgombea ubunge Maswa mashariki- ccm
wanachama na wananchi mbalimbali wakimsindikia kurudisha fomu ya kugombea ubunge jimbo la maswa mashariki

Kwa upande  wake  katibu  wa  ccm  Mkoa  wa  Simiyu  ndugu  Eva Michael  Degeleki  amewataka  wanachama  wa  chama  hicho kuvunja  makundi  na kuwa  na  kundi moja litakalofanikisha ushindi katika uchaguzi mkuu ngazi   za madiwani,  wabunge  na  Rais

sauti ya Eva Degeleki katibu wa ccm mkoa wa simiyu
picha ni matukio mbalimbali wakati wa urejeshaji wa fomu za kuwania Ubunge maswa mashariki