Sibuka FM

Bifu la Mpina na Bashe, Rais Samia apigilia msumari

18 June 2025, 2:43 pm

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa wilaya ya Meatu

Maombi hayo kuyaleta mbele ya Rais ni kujitafutia umaarufu na kudhibitisha mbunge hakulifanyia haki jimbo lake ” Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akiwa wilayani Meatu-Simiyu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia suluhu Hassani ameonyesha kukerwa na changamoto alizoziwasilisha katika mkutano wa hadhara Mbunge wa Jimbo la Kisesa Wilayani Meatu Mkoani Simiyu na kusema kuwa changamoto hizo alipaswa kuziwasilisha Bungeni ili zifanyiwe kazi na Mawaziri wa kisekta.

Mh Samia amesema kuwa mbunge ameshindwa kulitendea haki jimbo lake na badala yake kusema kuwa Kisesa bado tunamdai Rais samia wakati Serikali imefanya kazi kubwa katika Jimbo lake

Sauti ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

Akiwasilisha salamu kwa niaba ya wananchi wa jimbo la kisesa mbunge wa jimbo hilo Mh Luhaga Mpina amesema ni vizuri suala la ununuzi wa Pamba lisiwe la mnunuzi mmoja kwani linaondoa sera ya soko huria pia hakuna ushindani huku akisema kisesa bado inamdai Rais Samia

Sauti ya Luhaga Mpina mbunge wa Kisesa
Mhe Luhanga Mpina – mbunge wa Kisesa

Waziri wa Kilimo mhe Hussein Bashe amesema amesema hata wanunuzi wakiwa wengi bei ya pamba inapangwa na Serikali na siyo wanunuzi huku akimtaja Mpina kuwa alichangia kuua kitalu cha mbegu cha Mwabusalu hivyo hatawavumilia wanasiasa wenye nia Ovu ya kuharibu zao la Pamba

Sauti ya Hussein Bashe – Waziri wa Kilimo
Hussein Bashe – Waziri wa Kilimo
Wananchi wa Meatu wakiwa katika mkutano wa hadhara wakimsikiliza Rais Dkt Samia Suluhu