Sibuka FM
Sibuka FM
14 June 2025, 10:09 am

Imebainishwa kuwa ongezeko la ajali za barabarani wilayani Maswa mkoani Simiyu,umetajwa kusababishwa na waendesha bodaboda wasiojua sheria za usalama barabarani hali iliyomlazimu mkuu wa Wilaya hiyo kukutana na bodaboda hao.
Na Alex Sayi
Baadhi ya waendesha bodaboda wilayani Maswa mkoani Simiyu walia na elimu za usalama barabani kwa madai ya marejesho kwa mabosi wao yanawafanya wafukuzane na muda hali inayowapelekea wasizingatie sheria na alama za barabarani
Akizungumza na bodaboda hao Mkuu wa Wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu Dkt Vicent Naano Anney amewataka maafisa Usafirishaji hao kuhakikisha wanashirikiana na Jeshi la polisi nakuwahimiza kuunda vikundi ili waweze kukopeshwa Pikipiki
Aidha Mkuu wa Usalama barabarani wilayani hapa, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi James Nyorobi amewataka waendesha boda boda kuzingatia sheria za barabarani ikiwemo kuvaa kofia ngumu, na kuzingatia matumizi ya taa za kuongozea magari
