Sibuka FM
Sibuka FM
22 May 2025, 2:02 pm

Migogoro mingi ya Wanandoa inasababishwa na kutokuandika Wosia inapotokea mume amefariki Dunia ndugu wa mwanaume wanakuja juu na kumdhurumu mali mjane aliyeachwa na marehemu wakati mali hizo wamezitafuta wawili hao. ” Dc Dkt Vicent Anney “
Wananchi wa kata za Sangamwalugesha, Dakama na Lalago zilizopo Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu wameshindwa kujizuia na kutoa kero zao kwa Mkuu wa Wilaya hiyo wakati wa Mkutano wa hadhara wenye lengo la kusikiliza kero mbalimbali za Wananchi
Wananchi hao wameeleza kuwa kumekuwepo na changamoto za soko, Mirathi na Upimaji wa ardhi katika maeneo yao hivyo wakamuomba Mkuu wa wilaya azishughulikie changamoto hizo ili wananchi waendelee kuwa na imani na Serikali yao
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndugu Maisha Mtipa na Rukia Saidi kutoka Mama Samia Legal Aid wakatoa Ufafanuzi na kuwaondolea hofu wananchi wa Sangamwalugesha, Dakama na Lalago kuhusu Masuala ya kuanzisha Soko, Msaada wa kisheria na Migogoro ya Ardhi
Kisha Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe Dkt Vicent Naano Anney akatoa maagizo ya Serikali kuhusu changamoto zilizowasilishwa na Wananchi ikiwepo kupeleka Umeme katika shule ya Msingi Mwanindo ifikapo Augost 30, 2025

