

20 March 2025, 12:21 pm
Nendeni mkasimamie haki na Stahiki za walimu wenzenu huko vijijini, kuna walimu wengi wananyanyasika na kudhurumiwa haki zao nyie viongozi mkawe chachu na siyo kikwazo na Kuwanyanyasa wenzenu walio chini yenu. ” Dc Anna Gidarya”
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe Anna Gidarya ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Itilima Mkoani Simiyu amewata viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania CWT Wilaya ya Maswa waliochaguliwa kuhakikisha wanaenda kutatua changamoto za Walimu hasa maeneo ya pembezoni mwa Mji.
Mhe, Gidarya amesema hayo alipokuwa Mgeni rasmi katika Uchaguzi wa Viongozi wa cwt Maswa na kusema kuwa walimu wanachangamoto nyingi sana huko vijijini zinazohitaji kutatuliwa na zingine kufikishwa mamlaka za juu zaidi ili kutafutiwa ufumbuzi na siyo kwenda kuwanyanya na kujifanya Mungu watu.
Mhe Gidarya ameongeza kuwa cwt malengo yake makubwa ni pamoja na Kusimamia na kutetea haki za walimu hivyo viongozi waliopatikana wakasimamie Masilahi ya walimu na kuwa na Umoja katika kazi zao huku akiwataka kuzisoma sheria za Utumishi wa Umma na kuzielewa ili kuepuka migogoro na waajiri wao.
Akitangaza matokeo ya Uchaguzi wa Viongozi wa nafasi mbalimbali katika Chama hicho, Katibu wa cwt Mkoa wa Simiyu Lucy Masengenya amesema katika nafasi ya Mwenyekiti aliyechaguliwa ni Zacharia s. Munubi kwa kura 153 kati ya kura 186 zilizopigwa akiwashinda Eliud k. John aliyepata kura 14, akifuatiwa na Mathew Kamalamo aliyepata kura 10, nafasi ya nne ni Ally Sadi alipata kura 4, nafasi ya tano ni Joseph Shabenesho kura 3 huku nafasi ya mwisho wakigongana wawili Silvester Butabu Edward na Godi Kiduma waliopata kura 1
Katika nafasi ya mweka hazina cwt Maswa alichaguliwa Chesta Kombe kwa kura 147 akifuatiwa na Lesta Lucas (12), Moses Lameshi (9), Saguda Kulwa (8) na Taraba b. taraba (5) huku kundi la Uwakilishi ( KE ) akishinda Devotha Soko aliyepata kura 93 akifuatiwa na Advelah Kashenya aliyepata kura 71 na Chiku Mohamed akipata kura 22.
Baada ya Uchaguzi mwenyekiti aliyechaguliwa akawashukuru wajumbe wote wa Mkutano kwa kumchagua tena kwa mara nyingi ili aendelee kuwatukia na kuwaahidi kuendeleza alipoishia huku akiwaomba ushirikiano katika kutimiza Majukumu yake.