Sibuka FM

Wananchi Maswa wapongeza zoezi la upigaji kura uchaguzi serikali za mitaa

27 November 2024, 4:03 pm

Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe, Aswege Kaminyoge akipakwa wino baada ya kumaliza kupiga kura mapema hii leo.

Wananchi  Wilayani   Maswa  Mkoani   Simiyu  Wameipongeza  Serikali   kwa  Mandalizi  Mazuri  ya  zoezi  la  Uchaguzi  wa  Serikali  za  Mitaa  uliofanyika  leo  Nov,  17, 2024

Wakizungumza  kwa  nyakati tofauti  baada  ya  kupiga  kura  wamesema  kuwa   wananchi  wamehamasika  kupiga  kura  kwa  Wingi  ili  kuchagua  Viongozi  katika  Maeneo  yao   kulingana  na  Mazingira  rafiki  ya  kupigia  kura  yaliyowekwa  na  Serikali.

Sauti za baadhi ya Wananchi Wilayanii Maswa

Maisha  Mtipa  ni Msimamizi  wa  Uchaguzi   Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa  amesema  kuwa  zoezi  linaenda  Vizuri  hajapokea  changamoto  yoyote  katika  Upigaji  wa  Kura   na  Vituo  vimefunguliwa  kwa  Wakati  licha  ya  kuwepo  kwa  changamoto  ya  Mvua.

Sauti ya Maisha Mtipa Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

Kwa  upande  wake  Mbunge  wa  Jimbo  la  Maswa  Mashariki  na  Naibu  Waziri   wa  Nchi, Ofisi  ya  Rais ,  Mipango  na  Uwekezaji  Mhe  Stanslaus  Nyongo  amesema  kuwa   Zoezi  limekuwa  na  Utulivu  wa  hali  ya  juu  huku  akitoa rai  kwa  wananchi  kujitokeza  kupiga  kura  na  kurudi  majumbani  ili  kusubiria  Matokeo

Sauti ya Stanslaus Nyongo baada ya kushiriki kupiga kura Uchaguzi serikali za Mitaa
Picha ni Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe Stanslaus Nyongo baada ya Kishiriki zoezi la Uchaguzi

Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa  Mhe,  Aswege  Kaminyoge ameshiriki  katika  kupiga  kura  katika  Kitongoji  cha  Mwantonja   kata  ya  Nyalikungu  Wilayani  hapa  na  kusema  kuwa  Zaidi  ya  Wananchi  Laki  moja  na  Hamsini  na  Tano  Elfu (155,000)  walijiandikisha   huku  kukiwa  na   Jumla  ya  Vituo  Mia  tano  na  kumi (510)  vya  kupigia  kura  katika  Uchaguzi  wa  Serikali  za  Mitaa.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa Aswege Kaminyoge