RC Kihongosi: Chagueni viongozi wenye sifa uchaguzi serikali za mitaa
29 September 2024, 10:16 am
Niwaombe sana wananchi wa Maswa msikubali kuhamasishwa na watu wenye nia ovu ya kuvuruga na uchochezi ili kuharibu amani kwani amani ikipotea wa kwanza kuumia ni watoto, akina mama na wazee.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mh Kenani Laban Kihongosi amewataka wananchi kuchagua Viongozi wenye Sifa za kuwaongoza na siyo kuchagua kwa Ushabiki na Upendeleo maana ndio wataoenda kuwatetea katika maamuzi ya ngazi za juu.
Mkuu wa Mkoa ametoa nasaha hizo kwa nyakati tofauti katika Mikutano yake ya hadhara Wilayani Maswa yenye lengo la Kusikiliza Kero za Wananchi na kuzitafutia Ufumbuzi ili Wananchi waendelee kuiamini Serikali yao.
RC Kihongosi ameongeza kuwa wananchi wasikubali kutumiwa na baadhi ya Wanasiasa ili kuvuruga Amani tuliyonayo kwa ajili ya Manufaa ya Watu Wachache ambao hawana Nia nzuri huku akitoleA ufafanuzi Suala la Watu kutekwa na Kutolewa Figo
Katika mkutano huo suala la changamoto ya Maji kuuziwa shilingi 50 hadi 60 kwa ndoo ya Lita 20 badala ya shilingi 40 likaibuliwa na Wananchi ambapo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Maswa (MAUWASA Mhandisi Nandi Mathias akatoa Ufafanuzi.
Baada ya Ufafanuzi huo Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mh Kihongosi akatoa maagizo hukusu Wananchi kupandishiwa gharama za Maji kiholela huku akiwataka waliopewa dhamana ya kuuza Maji kutowanyanyasa Wananchi kwa Kigezo cha Sungusungu
Mkuu wa Mkoa yupo katika Ziara ya Siku Sita kuanzia 26 Sept hadi 01 Oct, 2024 Wilayani Maswa kwa ajili ya kusikiliza Kero za Wananchi na kuzitafutia Ufumbuzi na zingine kuzibeba kwa ajili ya Ufuatiliaji Zaidi