RC Kihongosi aonya wanaotoa taarifa za taharuki kwa jamii
27 September 2024, 8:49 pm
Wananchi wilayani Maswa zipuuzeni taarifa za watoto kutekwa na kutolewa figo, hao ni wapotoshaji tu wenye lengo la kuondoa amani ya taifa letu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mh Kenani Laban Kihongosi ameonya watu wanaoeneza taarifa za Taharuki za Watoto kupotea,, kutekwa na Wengine kutolewa Figo..
Onyo hilo amelitoa kwa Nyakati Tofauti katika Mikutano yake ya Hadhara yenye lengo la kusikiliza kero za Wananchi na Kuzitafutia Ufumbuzi katika Kata za Dakama, Sangamwalugesha, Lalago na Mbaragane zilizopo Wilayani Maswa.
Mhe, Kihongosi amesema kumekuwepo na taarifa za Taharuki kwa Jamii kuhusu watu kutolewa Figo, Kutekwa na Watoto kupotea kitu ambacho siyo kweli kwani hamna hata mmoja aliyedhibitisha mtoto wake kutekwa na amewataka kulinda na kudumisha amani ya Nchi yetu.
Katika Ziara hiyo ya Mh Mkuu wa Mkoa , Wananchi walipata nafasi ya kuwasilisha Kero zao zinazowasumbua ikiwemo changamoto za Umeme, Barabara na Uhaba wa Watumishi katika Zahanati na Shule za Msingi na Sekondari
Meneja Tanesco Mkoa wa Simiyu Alistidia Clemence Kashemeza na Mkuu wa Division ya Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Dkt Lucy Kulong’wa wakatoa Majibu ya Serikali kuhusu Changamoto hizo.