Sibuka FM

Wananchi  Maswa  watoa Maoni  kuhusu  Dira ya Maendeleo  2025- 2050

15 August 2024, 10:40 am

Baadhi ya Wananchi na Viongozi mbalimbali wa Dini wakiwa katika Kikao cha Kutoa Maoni yao kuhusu Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 – 2050 katika Ukumbi wa Halmashauri Maswa Picha na Nicholaus Machunda

Wananchi  Wilayani  Maswa  Mkoani  Simiyu  wamepaza  sauti   zao  na  kutoa  Maoni  juu  ya  Dira  ya  Maendeleo ya  Taifa  ya  2025 – 2050  wakati  wa  Kikao  cha  Kamati  ya  Ushauri  ya   Wilaya – DCC   kilichofanyika  katika  Ukumbi  wa  Halmashauri  ya  Wilaya  hiyo.

Wamesema  kuwa  katika  Dira  ya  Maendeleo  ya   Taifa  ya   mwaka  2025 – 2050  Serikali  iboreshe   katika  Huduma  za  Afya,  Kilimo,  Mifugo,  Elimu na Miundombinu  ili  kukuza  uchumi  wa  Taifa.

Sauti za Wananchi Maswa wakitoa Maoni yao kuhusu Dira ya Maendeleo

Katika  kikao  hicho  kilichohusisha  wadau  mbali  mbali   wakiwemo  Viongozi  wa   Dini  nao  pia  wakasisitiza  Suala  la  Amani  na  Utulivu  katika  Nchi  ili  kukuza  Ustawi  wa  Taifa

Sauti za Viongozi wa Dini katika kutoa maoni

Akifungua  kikao  hicho  Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa  Mhe  Aswege  Kaminyoge  amesema  kuwa  Katika  Utekelezaji wa  Dira  Serikali  imefanya  Mambo  makubwa  ya  Maendeleo  kwa  Wananchi  katika  nyanja  mbali mbali ikilinganisha  na  miaka ya  zamani  kabla ya  Dira

Sauti ya Mkuu wa Wilaya ya Maswa
Picha: aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh Aswege Kaminyoge, Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mh Paul Maige na kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndugu Maisha Mtipa wakati wa Kikao cha kamati ya Ushauri ya Wilaya -DCC kuhusu ukusanyaji wa maoni ya Dira ya maendeleo ya Taifa

Emmanuel  Ludomya  ni  Mratibu  wa  Dira  ya  Maendeleo  ya  Wilaya  ya  Maswa akasema  maoni  yaliyotolewa  na  Wananchi watayafikisha  sehemu  husika  ili  Serikali  iyafanyie  kazi  kwa  Maendeleo  ya  Taifa.

sauti ya Mratibu wa Dira ya Maendeleo ya Wilaya Emmanuel Ludomya