Mpina agawa vifaa vya TEHAMA jimboni
13 August 2024, 10:47 pm
Nicholaus Machunda – Simiyu
Mbunge wa Jimbo la Kisesa lililopo wilayani Meatu mkoani Simiyu Mhe. Luhaga Joelson Mpina amekabidhi vifaa vya TEHAMA katika shule tisa za Sekondari jimboni kwake vyenye thamani ya Shilingi Milioni 22. 5 ili kusaidia Utendaji kazi na Kuongeza Ufaulu.
Akikabidhi Vifaa hivyo vya TEHAMA ikiwemo Mashine ya Kudurufu Karatasi (Photocopy Mashine ) na Komputa kwa ajili ya kusaidia Uandaaji wa Majaribio ya Mitihani kwa Wanafunzi na shughuli mbalimbali za Kiofisi huku akitaja gharama za kila kifaa
Aidha Mhe Mpina ametatua Changamoto ya Uhaba wa Matundu ya vyoo na Mfumo wa Umeme katika Shule ya Sekondari Mwakaluba baada ya kuelezwa kuwa shule hiyo ina uhaba wa Matundu ya Vyoo kwa Wanafunzi huku Walimu wakichangia Matundu hayo na Wanafunzi
Akimkaribisha Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Kaimu Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Meatu Mwl Antony Luyeye amesema kuwa Mhe Mpina amekuwa akijitoa sana katika kusaidia Idara ya Elimu hivyo wanampongeza na Kumshukuru sana
Akitoa taarifa fupi kwa Mgeni rasmi, Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwakaluba Mwalimu Woga Obadi Charles amesema kuwa changamoto kubwa katika shule hiyo ni Uhaba wa Matundu ya vyoo baada ya kutitia vile vya awali kutokana na Mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha .
Mwalimu Makinga Bulenya ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Kisesa ambapo ni Miongoni mwa shule Tisa zilizopata Vifaa vya TEHAMA amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Kisesa Mhe, Luhaga Mpina kwa Ushirikiano anaotoa katika Kuinua Elimu Jimboni hapo.
Nao baadhi ya Wanafunzi waliozungumza na RADIO SIBUKA FM wamemshukuru Mbunge wao kwa kuleta Vifaa hivyo vya TEHAMA na kumuahidi kufanya vizuri katika Mitihani yao na Kuongeza Ufaulu