Sibuka FM

TRA watoa siku 14 wafanyabiashara kuwa na mashine za EFD Maswa

29 May 2024, 3:04 pm

Pichani wa katikati ni mkuu wa wilaya ya Maswa , Aswege Kaminyoge kulia kwake ni meneja TRA na kushoto ni katibu tawala wilaya wakiwa kwenye kikao Cha wafanyabiashara na TRA Picha na Nicholaus Machunda

Ukikwepa kulipa kodi maana yake umekubali kuliingizia hasara Taifa lako na kupelekea kudumaza shughuli za kimaendeleo tulipeni kodi kwa hiari kwa kutoa EFD mashine kwa waliokidhi vigezo.

Na,Daniel Manyanga 

Mamlaka ya mapato nchini TRA wilaya ya Maswa mkoani Simiyu imetoa siku kumi na nne kwa wafanyabiashara waliokidhi vigezo vya kuwa na mashine ya EFD kununua na kuanza kunitumia mara moja.

Akizungumza na wafanyabiashara wa wilaya ya Maswa wakati akitoa elimu ya kulipa  kodi kwa hiari meneja wa TRA wilayani hapo, Lucius Theonesti amesema kuwa kuna baadhi wa wafanyabiashara wamekidhi vigezo vya kutumia mashine za EFD listi lakini bado hawatumii katika shughuli zao hivyo wamewaandikia barua ikiwataka ndani ya siku kumi na nne wawe na mashine hizo na kuanza kuzitumia.

Sauti ya meneja TRA akitoa agizo la siku kumi na nne

Theonesti ameongeza kuwa kwa mfanyabiashara ambaye amefikia mauzo ya kiasi cha shilingi milioni kumi na moja kwa mwaka ndiye anapaswa kuwa na mashine ya EFD ikiwa na mchanganuo wa mauzo ya shilingi elfu thelathini na sita kwa siku huku waliochini ya mauzo hayo wakitakiwa kutumia vitabu vya mahesabu kwenye biashara zao.

Sauti ya meneja wa TRA wilaya akitoa elimu kwa wafanyabiashara

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge amewataka TRA kuendelea kutoa elimu ya sheria ya mlipa kodi kwa wafanyabiashara ili kuondoa sintofahamu ambazo zinajitokeza wakati wa ukadiliaji wa kodi hizo.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Maswa akizungumza na wafanyabiashara

Aswege Kaminyoge amesema kuwa swala la kutoa na kudai EFD mashine lipo kisheria hivyo amewaomba wafanyabiashara waliokidhi vigezo kutoa lisiti  pindi wanapouza na kununua bidhaa.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Maswa akitoa maelekezo kwa TRA kuendelea kutoa elimu ya kidi

Chagu John na Zainab Masoud ni baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria kikao hicho ambapo wameomba TRA kutumia lugha rafiki na ya kueleweka na kuwatembelea ili kujionea changamoto ambazo wanazipitia katika biashara zao.

Sauti za wafanyabiashara wakizungumza kwenye kikao