Wanane mikononi mwa polisi kwa dawa za kulevya Simiyu
19 May 2024, 5:52 pm
Hatutasita kukuchukulia hatua kali za kisheria kwa wale ambao wanajihusisha na uhalifu maana mkono wa serikali ni mrefu hivyo njia sahihi ni kuachana na vitendo vya uhalifu
Na, Daniel Manyanga
Jeshi la polisi mkoani Simiyu linawashikilia watu wanane kwa tuhuma za kukamatwa na dawa za kulevya kati ya watuhumiwa mia moja arobaini na nane katika kipindi cha mwezi april mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu,kamishina msaidizi wa polisi(ACP) Edith Swebe amesema kuwa katika kipindi cha mwezi april jeshi la polisi walifanya oparesheni ya kukamata dawa za kulevya na kufanikiwa kukamata watuhumiwa wanane pamoja na magari manne ambayo yalikuwa yanatumika kusafirishia katika wilaya za Maswa na Busega mkoani hapo.
Swebe ameongeza kuwa katika kipindi cha mwezi april walifanikiwa kukamata watuhumiwa mia moja na arobaini na nane kwa matukio mbalimbali yakiwezo wizi,ujangili na madawa ya kulevya.
Katika hatua nyingine ACP Edith Swebe ametoa wito kwa wananchi mkoani hapo kuacha kujihusisha na matukio ya kihalifu ambayo yanayoweza kuwaweka katika mikono ya jeshi la polisi huku akiwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiaano ili kukomesha vitendo vya uhalifu.