Sibuka FM

Wananchi mjini Maswa na vijiji 15 kukosa maji kwa siku mbili

18 May 2024, 6:20 pm

Pichani ni mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Maswa (MAUWASA), Mhandisi Nandi Mathias akizungumza na waandishi wa habari Picha na Daniel Manyanga

Mpango wa kuwapatia maji safi na salama ni sera ya wizara ya maji hivyo jukumu la kukosekana kwa huduma ya maji kwa wananchi pindi usafi au kutibu maji ni kuboresha huduma hiyo.

Na, Daniel Manyanga 

Wananchi mjini Maswa na vijiji 15 wilayani Maswa mkoani Simiyu watakosa huduma ya maji safi na salama kwa muda wa siku mbili ili kupisha zoezi la usafi wa tenki la maji la ardhini lililopo kwenye chanzo kikuu cha maji katika bwawa la Zanzui.

Pichani ni muonekano wa nje wa jengo la mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Maswa (MAUWASA) Picha na Daniel Manyanga

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo hii ofisini kwake mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Maswa (MAUWASA),Mhandisi Nandi Mathias amesema kuwa kukosekana kwa huduma ya maji safi katika mji wa Maswa na vijiji kumi na tano ni kupisha zoezi la kufanya usafi katika tenki la ardhini lililopo kwenye chanzo kikuu cha maji katika bwawa la Zanzui.

Sauti ya mhandisi Nandi Mathias akielezea sababu za kukosekana kwa huduma ya maji

Mhandisi Nandi amesema kuwa zoezi hilo linatarajiwa kuanza siku ya Jumapili ya tarehe 19 hadi Jumatatu ya tarehe 20 kwa mwezi huu wa tano hivyo wakazi wa mjini Maswa na vijiji kumi na tano ambavyo vinatumia maji ya MAUWASA watakosa huduma hiyo.

Sauti ya mhandisi Nandi Mathias akielezea muda utakaotumika katika kazi hiyo

Mhandisi Nandi Mathias amewataka wananchi kutumia maji kwa umakini katika kipindi hichi ambapo huduma ya maji safi na salama itakuwa haipatikani katika maeneo hayo.

Sauti ya mhandisi Nandi Mathias akitoa wito kwa wananchi kutunza maji

Kwa upande wake Paul Yohana na Samwel Mwanga ni wakazi wa mjini Maswa na watumiaji wa huduma ya maji safi na salama wamesema kuwa kutokana na kukosekana kwa maji siku mbili haiwezi kuwa na athari kubwa hivyo MAUWASA iweze kufanya zoezi hilo kwa muda ambao wamepanga au chini ya hapo ili wananchi waendelee kupata huduma ya maji safi na salama.

Sauti za wananchi na watumia huduma ya maji mjini Maswa