Sibuka FM

Bei ya pamba haina tija kwa wakulima wa Bariadi

14 May 2024, 9:34 am

Pichani ni mwenyekiti wa baraza la madiwani wilayani Bariadi mwenye kipaza sauti akiongoza kikao cha baraza hizo picha kutoka maktaba

Kutokana na bei ya pamba kuwa ndogo katika msimu wa kilimo wa mwaka 2024/25 iliyotangazwa mkoani Shinyanga wakulima wameanza kuangalia namna ya kuachana na kilimo hicho.

Na, Daniel Manyanga

Baraza la Madiwani la halmashauri ya wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu limeiomba serikali kutazama upya bei elekezi ya pamba ya msimu wa mwaka 2024/25 iliyotangazwa mkoani Shinyanga ambayo ni  shilingi 1150  kwa kg moja licha ya kuongezeka shilingi 90 ikilinganishwa na msimu wa mwaka jana ili iendane na gharama halisi alizotumia mkulima wa zao hilo.

Mganga Kanagana ni diwani wa kata ya Ngulyati na Maduka Mashaurimapya diwani wa kata ya Mwadobana wamesema kuwa bei iliyotangazwa na serikali ya msimu wa mwaka 2024/2025 haiendani na gharama halisi ambazo anatumia mkulima hivyo ni vyema serikali akalitazama upya ili kuweza kuleta ushindani kwa wakulima wa pamba pamoja na kuleta tija.

Sauti ya madiwani wakiomba serikali kuangalia upya bei ya pamba

Madiwani hao wameongeza kuwa gharama za zao la pamba mpaka kufikia hatua ya kuiva na kuvuna zipo juu hali ambayo inapelekea baadhi ya wakulima kufikiria kuacha kujihusisha na kilimo cha pamba kutokana na kutokupata faida linapokuja swala la bei kupangwa bila kushirikishwa wakulima wenyewe.

Sauti ya madiwani wakizungumzia swala bei kutokuwa na tija kwa mkulima

Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi,Mayala Lucas amesema kuwa kilimo cha pamba ni uti wa mgongo mkoani hapo na kuongeza kuwa msimu huu mavuno yatakuwa machache ikilinganishwa na misimu mingine.

Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Bariadi