Wadau: Miaka 60 ya muungano, Maswa haikuwa hivi
27 April 2024, 10:32 am
Kongamano la Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kuwa Tanzania limefanyika Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa na Kuhudhuriwa na Wadau Mbalimbali
Nicholaus Machunda
Wadau wa Maendeleo Wilayani Maswa Mkoani Simiyu Wamesema kuwa Miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na Kuunda Jina la Tanzania Umekuwa na Mafanikio Makubwa na Umerahisisha Upatikanaji wa Huduma kwa Wananchi.
Akihutubia katika Kongamano lililofanyika Katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa, Mkuu wa Wilaya hiyo ambaye ndie alikuwa Mgeni Rasmi katika Sherehe hizo Mhe, Aswege Kaminyoge asema kuwa Maswa ya sasa siyo kama ile ya Miaka ya Nyuma.
Kamiyoge amesema katika sekta mbalimbali mabadiliko Makubwa yamefanyika na Wananchi wamesogezewa Huduma kwa Ukaribu zaidi ikilinganishwa na hapo awali ambapo Wananchi walikuwa wanasafiri Umbali Mrefu Kufuata Huduma Muhimu za Kibinadamu.
Akitoa Ufafanuzi wa Maadhimisho hayo ya Miaka 60 ya Muungano, Mwenyekiti wa Sherehe hizo ambaye pia ni Katibu Tawala wa Wilaya Athuman Kalaghe amesema lengo la Muungano lilikuwa zuri hivyo ni vizuri kuenzi na Kuuudumisha.
Mzee Sospeter Msuluja ni Mwalimu Mstaafu amesema amesema zamani hali haikuwa kama ilivyo sasa kwani Maendeleo yanaonekana kila Kona na Kuwataka Watumishi Waliko makazini Waendelee Kuwatumikia Wananchi kwa Ueledi Mkubwa na Uzalendo.
Aidha Kongamano hilo limehudhuriwa na Wadau mbalimbali Wakiwemo Wakuu wa Taasisi na Wanafuzi kutoka Shule za Msingi na Sekondari nao wakawa na haya yakusema kuhusu Miaka 60 ya Muungano.