TEHAMA mashuleni kuongeza ufaulu kwa wanafunzi Maswa
26 April 2024, 4:24 pm
Vifaa vya tehama sasa kusaidia ujifunzaji kwa wanafunzi shuleni nakuwasaidia walimu kwendana na wakati uliopo kwa sasa wa sayansi na teknolojia hivyo kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Na,Paul Yohana
Mkuu wa wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Aswege Kaminyoge amekabidhi vifaa vya tehema kwa maafisa elimu kata na wakuu wa shule ambavyo vitatumika mashuleni ili kuongeza ujuzi kwa wanafunzi na kuendana na mabadiliko ya teknolojia.
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi vifaa hivyo, Aswege Kaminyoge amesema kuwa vifaa hivyo vina gharama kubwa hivyo basi wanatakiwa kuvitunza kama mboni ya jicho kwa kushirikiana na maafisa elimu na wakuu wa shule ili viweze kudumu na kuleta tija kwa wanafunzi ambao wanaenda kuvitumia haswa kwenye kuongeza ufaulu.
Vivian Christian ni kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Maswa amesema kuwa vifaa hivyo wamevipokea kutoka mkoani na vitapelekwa kwenye shule mbili za Binza na Malampaka na kutaja vifaa hivyo ni kompyuta mpakato (4) smart tv mbili inch 65 pamoja na kamera 2.
Kwa upande wake afisa elimu msingi wilaya ya Maswa Dkt.Lucy Kulongw’a amesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia katika kuongeza ujifunzaji kwa wanafunzi hivyo basi wakuu wa shule wakavitumie huko mashuleni na siyo kuviweka ndani kama mapambo.