Mfumo wa stakabadhi ghalani kuwanufaisha wakulima Simiyu
16 April 2024, 10:04 am
Na Nicholaus Machunda
Wakulima Mkoani Simiyu wapata mwarobaini wa bei ya mazao baada ya kilio cha muda mrefu cha kukosa soko la uhakika
Wananchi Mkoani Simiyu Wameishukuru Serikali Kuruhusu kuuza Mazao yao ya Nafaka kupitia Mfumo wa Stakabadhi Ghalani kuwa Umekuwa na faida kwao huku ukilenga kumkomba Mkulima.
Laurensi Masunga Chajo ni Mkulima kutoka Wilaya ya Meatu Mkoani hapa amesema kuwa mfumo huo ni mzuri kwani unafaida kwa Mkulima na utamkomboa kiuchumi
Kwa Upande wake Japheti Magulyati ni Mkulima kutoka Maswa anaishukuru Serikali kwani mfumo huo umewanufaisha zaidi ikilinganishwa na hapo awali ambapo bei ya choroko ilikuwa haieleweki
Akitoa Ufafanuzi juu ya Bei ya Mnada katika Zao la Choroko na Faidi watakayopata Wakulima kupitia Bei hiyo, Mwenyekiti wa Chama Kikuu cha Ushirika Mkoa wa Simiyu (SIMCU) Ndugu Lazaro Walwa amesema bei ya Ushindanishi ni nzuri na Faida inayopatikana inarudi kwa Wakulima
Aidha ndugu Walwa ametoa rai kwa Wakulima kupeleka Choroko kwenye vyama vya Msingi vya Ushirika (AMCOS ) kwani kuna tofauti kubwa kati ya Bei ya Mtaani na Bei ya Mfumo wa Stakabadhi Ghalani