DC KAMINYOGE ; Wananchi Jitokezeni kwenye Mikutano ya Hadhara
3 April 2024, 10:20 am
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Mhe, Aswege Enock Kaminyoge amewataka Wananchi wilaya hapo kujitokeza kwa Wingi katika Mikutano ya Hadhara inayoitishwa na Viongozi wao wa Vijiji na kata ili kutoa kero zao na changamoto mbalimbali zinazowakabiri.
Mh Kaminyoge amesema Mikutano ya Hadhara ndio sehemu sahihi ya kupata taarifa za maendeleo ya vijiji na utatuzi wa changamoto zake lakini pia ni Utekelezaji wa Dhana ya Utawala Bora
Aidha Mh Kaminyoge amezitaka Taasisi zote za Serikali kuhakikisha wanapima na Kutambua mipaka ya maeneo yote ili kuepuka Migogoro ya Mipaka dhidi ya Wananchi hivyo maeneo yote yaliyovamiwa na Wananchi yarudishwe mara moja
Akitolea Ufafanuzi malalamika yaliyo yaliyotolewa na Wananchi juu ya Utaratibu wa Matibabu ya Bima ya Afya iliyoboreshwa CHF Muuguzi Mfawidhi wa Zahanati ya Bugalama Tumpe Mkussa amesema Utaratibu wa CHF mwanacha anapaswa kutibiwa mara tatu hadi mara Nne kwa Mwezi
Ngude Balunhya ni Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Bugalama , kata ya Bugalama Wilayani Maswa amesema wananchi wengi hawahudhurii Mikutano ya Hadhara hivyo baadhi yao kuuliza Maswali yaliyofanyiwa Utatuzi likiwepo suala la Wafugaji kutozwa fedha kubwa ya Kuoshea Mifugo yao.
Awali baadhi ya Wananchi wa Bugalama walipaza sauti zao za Kero kwa Mkuu wa Mkuu wa Wilaya ya Maswa na Kumuelezea Kero ya Watendaji wanaokula Fedha za Wananchi kisha kuhamishiwa kwenye Vituo vingine bila Kuchukuliwa hatua zozote huku Mkuu wa Wilaya akitoa maelekezo kwa Mtendaji aliyehamishwa Kurudi kweney Kijiji hicho