DC Kaminyoge atoa ufafanuzi changamoto ya sukari wilayani Maswa
28 February 2024, 11:15 am
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Mh, Aswege Kaminyoge ametoa ufafanuzi kuhusu Changamoto ya Kupanda kwa bei ya Sukari na kutoa maelekezo ya Serikali kuhusu upatikanaji wa Bidhaa hiyo.
Kaminyoge amesema hayo wakati akizungumza na Wafanyabiashara wa Maswa na kusema kuwa baada ya kufanya utafiti alingua kati ya Wafanyabiashara wa Maduka ya Jumla Saba aliowatembelea ni Wafanyabiashara Wawili tu ndio Walioonyesha Risti za Manunuzi ya Sukari kwa Wauzaji wakubwa.
Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa Serikali imeshatoa bei elekezi kwa Bidhaa hiyo hivyo ni vizuri Wafanyabiashara Wakawa Wazalendo kwa Kufuata bei hiyo ili kuepuka kuwanyonya Watumiaji ambao ni Wananchi wa Kawaida
Baadhi ya Wafanya biashara walipaza sauti zao kwa Mkuu wa Wilaya na kuelezea Kero mbalimbali ikiwemo Milango katika Machinjjio ya Nyama, Dampo la kutupia Uchafu, Vitambulisho wa Wajasilia mali, Huduma za Matibabu kwa Wazee.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Ndugu Maisha Mtipa amesema kuwa atatekeleza yote waliyokubalian hivyo kila Mtu atimize wajibu wake katika kufanikisha na kuahidi kufanya kikao kingine kwa kutoa elimu zaidi kwa wafanyabiashara,.
Robert Gunda ni miongoni wa Wafanyabiashara katika Soko kuu la Maswa amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kufika na kusikiliza kero za kwani muda mrefu walikuwa hawajui wapi pakupekeleza Changamoto zao.