Baraza la madiwani laridhia kuvunjwa mamlaka ya mji mdogo Maswa
18 February 2024, 3:43 pm
Na Nicholaus Machunda
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kwa Kauli moja limeridhia kuvunjwa kwa Mamlaka ya Mji mdogo Maswa kwakushindwa kukidhi vigezo na Kuazimia kuanzisha Mchakato wa Kupata Halmashauri mbili.https://maswadc.go.tz/
Azimio hilo lilitolewa na Mkrugenzi Mtendaji wa Halmashauri wa Wilaya ya Maswa Ndugu Maisha Mtipa katika kikao cha Baraza la Madiwani Robo ya Pili ya Mwaka wa Fedha 2023/2024 na Wajumbe wa Kikao hicho kuridhia azimio hilo na kuruhusu kuanzisha mchakato wa Halmashauri nyingine.
Paul Simon Maige ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu amesema kuwa kumekuwa na gharama kuwa za uendeshaji wa Mamlaka ya Mji mdogo hivyo kupelekea kuipa Mzigo halmashauri ya Wilaya kwani Mamlaka hiyo ilishindwa kujiendesha kwa mapato yake
Aidha Mhe, Maige amesema kuanzishwa kwa Halmashauri mbili katika wilaya moja itasaidia kusogeza kuduma kwa Wananchi pamoja na kuongeza ajira kwa Vijana kwani kutakuwa na Ongezeko la maeneo ya kiutawala na nafasi mbalimbali zitahitaji Watu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Maswa Ndugu Onesmo Makota amesema uamuzi uliofanywa na Waheshimiwa Madiwani ni Mzuri kwani unalenga kusogeza huduma kwa Wananchi kama ilivyo azima ya Mh Rais Samia.
Mmoja wa Diwani wanaounda Mamlaka ya Mji mdogo Maswa Masanja Mpiga asema wamefikia Uamuzi huo kutokana na Kkushindwa kukidhi vigezo kwa Muda mrefu toka kuanzishwa Mamlaka hiyo Miaka Kumi iliyopita.
Katika kikao hicho Madiwani walipata nafasi za kuchangia agenda mbalimbali ikiwemo suala la Kusimamia na kuongeza Mapato ya Halmashauri ya Maswa