Mkuu wa Wilaya akanusha taarifa za Nyumba 112 kobomoka kufuatia Mvua zinazoendelea kunyesha
5 February 2024, 11:58 am
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Mkoani Simiyu Mhe, Aswege Kaminyoge amekanusha taarifa iliyotolewa kwenye vyombo vya habari kuwa nyumba 112 zilibomolewa na mvua kubwa iliyonyesha Tarehe 27/01/ 2024 katika kata ya Mbaragane na kusema kuwa ni nyumba 5 tu zilizobomoka kutokaa na Mvua hiyo.
Amesema kuwa kwa mjibu wa sheria No 6 ya Maafa ya mwaka 2022 na kanuni zake imewapa Mamlaka Viongozi wa serikali kama Vile Waziri mkuu kwa ngazi ya Taifa, Mkuu wa Mkoa kwa ngazi ya Mkoa na Mkuu wa Wilaya kwa ngazi ya Wilaya.
Aidha Mhe, Kaminyoge ameseammkuwa taarifa za tahadhari za uwepo wa Mvua kubwa kwa Mwaka zilitolewa mapema ili wananchi waweze kuchukua Tahadhari lakini wengi wao hawakufanya hivyo..