Meatu:wahadzabe waiomba Serikali kuwatengea makazi ya kudumu
1 February 2024, 2:15 pm
Wahadzabe wapatao (360 ) waishio kwenye kaya (46) kijiji cha Sungu Kata ya Mwabuzo Wilayani Meatu Mkoani Simiyu hawana makazi rasmi.
Na, Alex Sayi.
Wahadzabe waishio pembezoni mwa pori la akiba la Makao lililopo Wilayani Meatu Mkoani Simiyu wameiomba Serikali kuwatengea makazi ya kudumu.
Hayo yamesemwa mapema hii leo na baadhi ya Wahadzabe hao wakati wakizungumza na Sibuka fm Radio walipopata wasaa wakuzungumzia changamoto zinazowakabili
Samson Salehe amesema kuwa jamii ya kihadzabe kwa sasa haina makazi maalumu na wanalazimika kuishi kama wakimbizi,huku akiiomba Serikali itambue uwepo wa Jamii hiyo
Salehe aliongeza kuwa kwa sasa wanatamani kuona watoto wao wanapata fursa ya kwenda shule ili waweze kuelimika na kujikwamu na ugumu wa maisha unaowakabili kwa hivi sasa
Aidha Mayunga Muguli amesema kuwa Jamii ya Wadzabe kwa sasa inakabiliwa na ugumu wa maisha kwa kuwa hawaruhusiwi kuingia porini bila kuwa na kibali maalumu