Dalali, Nyerere jela miaka 30 kwa kubaka na kukutwa na dawa za kulevya
26 January 2024, 6:03 pm
Dalali na Nyerere Wahukumiwa Jela miaka 30 kila mmoja kwa makosa ya kubaka binti wa miaka 7 mwanafunzi wa darasa la kwanza na kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi kilo 35 zikiwa zimehifadhiwa nyumbani.
Na,Daniel Manyanga
Watu wawili mkoani Simiyu Wamehukumiwa miaka 30 Jela kila mmoja kwa makosa ya kubaka mwanafunzi wa darasa la kwanza na kukutwa na dawa za kulevya huku wengine 14 wakihukumiwa miaka 20 Jela kila mmoja kwa kukamatwa na nyara za serikali zikiwemo nyama ya Nyumbu,kichwa cha Nyati ,Vipande 12 vya nyama ya Twiga na Vichwa 12 vya mnyama Swala.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapo kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Simiyu ,ACP Edith Swebe, Amesema kuwa mtuhumiwa Daudi Dalali miaka 26 Msukuma , mkulima ,Mkazi wa Jashimba wilayani Maswa amehukumiwa kifungo cha miaka 30 Jela kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya aina ya Bangi kilo 35 akiwa amedhihifadhi nyumbani kwake katika mtaa wa Jashimba.
ACP Swebe ameongeza kuwa mtuhumiwa Nyerere Shidute amehukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa kumbaka binti mwenye miaka 7 mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Mwampala tukio lililofanyika kijiji hapo kata ya Kilalo wilaya ya Bariadi.
Aidha ACP Swebe amesema kuwa kwa kipindi cha mwezi mmoja jumla ya watuhumiwa 148 walikamatwa na wengine wamehukumiwa tayari huku baadhi yao mashauri hapo katika hatua mbalimbali za kisheria.
Jeshi la polisi mkoani hapo limetoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuweza kubaini matukio ya kihalifu huku likitangaza kuendelea na oparesheni ya usalama barabarani kwa watumiaji wote wa vyombo vya moto.