Kamati ya siasa Maswa yaridhishwa utekelezaji miradi ya maendeleo
2 December 2023, 7:44 am
Kamati ya Siasa ya chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Maswa ikiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Ndugu Onesmo Makota Imetembelea na Kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo inayotekelezwa katika Jimbo la Maswa Magharibi.
Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa na Kamati hiyo ni Ujenzi wa Tanki la Maji katika Mji wa Malampaka, Ujenzi wa Zahanati Nyabubinza, Mradi wa Umeme Vijijini (REA), Mradi wa Maji Mwatumbe na Matengenezo ya Barabara kutoka Malampaka hadi Mwanh’onoli na Kuridhishwa na Miradi hiyo.
Akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Tanki la Maji katika Mji wa Malampaka Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira mjini Maswa (MAUWASA ) Mhandisi Nandi Mathias amesema kuwa mradi huo wa dharura utanufaisha Wakazi zaidi ya Elfu kumi na tatu.
Naye Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mhe, Mashimba Ndaki amewataka MAUWASA kukamilisha haraka mradi huo ili kuondoa changamoto ya Upatikanaji Maji katika mji huo ambao unakua kwa Kasi sana.
Ikiwa katika kata ya Shishiyu kijiji cha Mwatumbe kamati ya Siasa imekagua chanzo cha maji kilichojengwa na RUWASA kupitia mdau wa Maendeleo WORLD VISION na kushauri kuwa Jumuiya za watumia Maji kupewa Elimu zaidi juu ya Uendeshaji na Utunzaji wa Mradi huo kwa ajili ya vizazi vijavyo na hapa katibu wa ccm Wilaya ya Maswa ndugu John Melele anaeleza..
Nao baadhi ya Wananchi Wameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Mh Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuleta miradi ambayo imesaidia kuondoa changamoto walizokuwa wanazipata hapo awali..