Maswa: Wazazi waaswa kuwasomesha watoto elimu ya ufundi
28 November 2023, 2:55 pm
Wazazi waaswa kuwasomesha Watoto wao Elimu ya Ufundi ili kukabiliana na obwe la ukosefu wa ajira uliopo Serikalini kwa hivi sasa.
Na,Alex Sayi.
Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mashimba Ndaki amewaasa wazazi/walezi kuwasomesha watoto wao Elimu ya Ufundi ili kukabiliana na soko la Ajira.
Hayo yamesemwa na (Mb)huyo wakati akiwahutubia wahitimu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Malampaka kilichopo Wilayani Maswa Mkoani Simiyu kwenye mahafali ya (47)ya Chuo hicho yaliyofanyika Novemba 24,mwaka huu kwenye Ukumbi wa Chuo hicho.
Mashimba ameongeza kuwa kuna haja ya Watoto kuwasomesha Elimu ya Ufundi ili waweze kujiajiri wenyewe badala ya kusubiria ajira Serikalini ,huku akiahidi kuwapatia mtaji wahitimu wa Chuo hicho
Diwani wa Kata hiyo Renatus Mashara amesema kuwa maisha ya sasa yanahitaji kuwa na Elimu na Elimu inayohitajika ni Elimu yakujitegemea,hivyo kutoa wito kwa wazazi kuwasomesha Watoto wao.
Mjumbe wa Bodi wa Chuo hicho Charles Buluge amewaomba wazazi na walezi wazawa wanaokizunguka Chuo hicho waone umuhimu wa kuwasomesha Watoto wao ili wapate Elimu itakayowasaidia kulima na Kufuga kisasa.
Mhitimu wa Chuo hicho na Rais wa Chuo hicho Charles Joseph amesema kuwa Elimu waliyoipata inawasaidia kujitegemea na kutokuwa tegemezi kwa Serikali na kwa wazazi.
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Wananchi Malampaka Michael Mahundi amesema kuwa anaishukuru Serikali ya awamu ya (6)kwa kukikumbuka Chuo hicho nakukitengea fedha za uboreshaji wa Chuo hicho.