Maswa:Kinamama waaswa kuchangamkia fursa za ufugaji wa samaki
26 October 2023, 5:48 pm
Kinamama toka jamii za wafugaji wameaswa kujiunga na chama cha wafugaji ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Na Alex Sayi.
Chama cha wafugaji Wilayani Maswa Mkoani Simiyu kimetoa wito kwa wanawake wanaoishi kwenye jamii za wafugaji kuchangamkia fursa za ufugaji wa Samaki ili kujikwamua kiuchumi.
Hayo yamesemwa na Katibu wa muda wa Chama cha Wafugaji Wilaya ya Maswa Mkoani hapa Bw,Samwel Nyarandu Kidima wakati akizungumza na jamii ya Wakulima na Wafugaji ili waweze kuchangamkia fursa zinazopatikana kwenye sekta hiyo ya Mifugo na kilimo.
Kidima akizungumza na Radio Sibuka amesema kuwa kunakila sababu ya Wafugaji na Wakulima kujiunga na chama hicho kuanzia ngazi ya Kijiji na Kata ili waweze kunufaika na uwepo wa chama hicho
Peter Paschal Mwenyekiti wa kikundi cha Agriween cha Wilayani Maswa Mkoani hapa amesema kuwa Agriween wanaendelea na mchakato wa kupata maeneo kwaajili ya mashamba darasa ili waweze kuwawezesha vijana kujifunza kwa vitendo.
Aidha Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani hapa David Ntinginya amesema kuwa vijana wanapaswa kubadiri fikra ili wajenge uwezo wa kujitegemea na kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza na Radio Sibuka fm kwa njia ya Simu Baba P wa Mwaukoli Meatu Mkoani hapa ambae ni Mkulima na Mfugaji amekiomba chama hicho cha Wafugaji kufika Vijijini waliko Wafugaji.