Maswa: Walimu Simiyu kunufaika na mafunzo ya elimu jumuishi
7 August 2023, 12:48 pm
Wizara ya Elimu,Sayansi na Technolojia kupitia Taasisi ya Elimu Nchini imewawezesha Walimu wapatao (50) kutoka shule za msingi 50 kupata mafunzo ya ufundishaji na ujifunzaji jumuishi.
Na,Alex Sayi.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa muda wa siku 4 ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa kupitia program ya Shule Bora yamefadhiliwa na Serikali ya Uingereza kupitia mfuko wa Uk,Aid.
Ester Malwa Mratibu wa Elimu bora ngazi ya Mkoa amesema kuwa mafunzo hayo yamelenga kuinua kiwango cha elimu jumuishi pamoja na kuweka mazingira mazuri yakujifunzia.
Malwa ameongeza kusema kuwa mafunzo hayo yanawajengea uwezo Walimu kuweza uwatambua watoto wenye mahitaji maalimu nakujua mbinu rafiki na jumuishi zakujifunzia.
Mwalimu Neema Makundi Afisa Elimu Taaluma Halmashauri ya Maswa na Mratibu wa Elimu bora Wilayani Maswa amesema kuwa anaishukuru Serikali kwakuwaletea mafunzo hayo kwakuwa yatasaidia wanafunzi wenye mahitaji maalumu kuweza kujifunza.
Mwl Salim Kidunda kutoka Shule ya Msingi Nyasosi Kata ya Ngulyati Wilayani Bariadi Mkaoni hapa alisema kuwa mafunzo hayo yamenisaidia kuanda dhana zakufundishia nakuwatambua watu wenye mahitaji maalumu.
Mwalimu Ferister Mkenda toka Shule ya Msingi Budalabujiga “A” alisema kuwa mafunzo haya yametusaidia walimu kwenda kuwasaidia wazazi walio na watoto wenye mahitaji maalumu.
Akizungumza na Radio Sibuka fm Frola Kisandu Mkazi wa Biafra Wilayani hapa amesema kuwa anaishukuru Serikali kwakuendelea kuboresha mazingira ya watoto wenye mahitaji maalumu kuweza kujifunza,huku akitoa rai kwa Serikali kuongeza idadi ya Walimu.