Waandishi Redio Jamii wapigwa msasa ushindani habari za mtandaoni
4 July 2023, 5:18 pm
Na,Alex Sayi
Waandishi wa habari na wahahiri wa Redio Jamii mikoa ya Kanda ya Ziwa wameshauriwa kuendana na mabadiliko ya uandaaji wa habari zenye ushindani kwenye mitandao ya kijamii.
Paschal Malulu mshiriki wa mafunzo toka Kahama Shinyanga amezungumzia umuhimu wa mafunzo hayo yaliyofanyika Gold Crest Hotel nakusema kuwa mafunzo hayo yamepanua uelewa kwa Waandishi ili kwendana na ulimwengu ulipo kwa sasa kwakuwa kwa sasa habari zimeridi kiganjani
kwa sasa habari zimeridi kiganjani
Zaituni Juma mshiriki na Mwandishi toka mkoani Tabora amesema kuwa mafunzo hayo yatawasaidia waandishi kuandaa habari zinazoweza kuwafikia watu wengi zaidi walio nje ya mikoa husika.
Kwa upande wake Amua Rushita mkufunzi toka Tanzania Development Information Organazatio(TADIO) amesema kuwa matumizi ya habari za mitandaoni umesaidia Radio za kijamii kuongeza wigo wa wasikilizaji walio nje ya mikoa yao.
Akizungumza wakati wa uhitimishaji wa mafunzo hayo Bi,Joan Kanza Afisa tathmini na ufuatiliaji mafunzo toka (TADIO) amesema kuwa mafunzo hayo yanajumuisha waandishi zaidi ya (25) toka Radio za kijamii Kanda ya Ziwa na kuongeza kuwa hadi sasa (TADIO) inahudumia zaidi ya redio (43) za kijamii nchini.