Simiyu: Watu 37 mikononi mwa jeshi la polisi kwa makosa mbalimbali
24 June 2023, 6:24 pm
Kwenye picha ni Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Simiyu ACP,Edith.M.Swebe akizungumza na Waandishi wa habari mkoani hapo
Na mwandishi,Daniel Manyanga
Jeshi la Polisi mkoa wa Simiyu limewatia mbaroni Watu (Watuhumiwa) 37 kwa makosa mbalimbali yakiwemo ya Ulawiti,Wizi ,Uvunjaji na Kupatikana na Nyara za serikali katika kipindi Cha kuanzia 25 May Hadi June 22 mwaka huu.
Hayo yamesemwa na kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Simiyu ACP Edith.M.Swebe wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini Kwake ambapo amesema kuwa Jeshi la polisi kwa kushirikiana na ofisi ya Taifa ya Mashtaka tayari wamefanikiwa kuwafikisha Mahakamani Watuhumiwa wa makosa hayo na kesi zao zikiendelea.
Sauti ya RCP Mkoa wa Simiyu,ACP Edith.M.Swebe
ACP Swebe ameongeza kuwa kufuatia oparesheni zinazofanywa na Jeshi la polisi mkoani hapo kwa kushirikiana na TANESCO walifanikiwa kuwakamata watu wawili wanaojihusisha na biashara ya vyuma chakavu wakiwa na nyaya za Cooper zenye uzito wa kilogram 53 nyaya hizo zinatokana na uharibifu na wizi wa miundombinu ya shirika la TANESCO kama Transformers hivyo shirika Hilo kulisababishia hasara ya shilingi milioni ishirini na Moja laki mbili na arobaini elfu.
Katika hatua nyingine Jeshi la polisi mkoani hapo limetoa onyo Kali kwa Wananchi wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu na kuwataka kuacha mara Moja kwani hatua kazi zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika anafanya vitendo vya uhalifu huku Wananchi wakitakiwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la polisi ili kuweza kuwabaini wahalifu wote na sheria iweze Kuchukua mkono wake.