Miradi mitatu iliyochunguzwa na Takukuru Simiyu yakutwa na dosari
2 June 2023, 7:16 pm
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoa wa Simiyu imebaini kuwa miradi 3 kati ya 14 yenye thamani ya zaidi ya bilioni 1 iliyofuatitiliwa imebainika kuwa na dosari katika utekelezaji wake .
Akitoa taarifa katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2022/2023 Januari hadi Marchi, 2023 Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Simiyu Aron Misanga amesema kuwa miradi iliyofuatiliwa inahusisha sekta za afya, elimu na barabara.
Sauti ya Aron Misanga
Naibu Mkuu wa Takukuru amesema kuwa jamii imekuwa na ushiriki mdogo katika miradi ya maendeleo hali inayopelekea miradi kujengwa chini ya kiwango na kutoleta tija na manufaa ya sasa na ya baadaye.
Sauti ya Aron Misanga
Katika hatua nyigine Takukuru mkoa wa Simiyu imefanya uchambuzi wa mifumo katika halmashauri ya Maswa, Meatu , Itilima na Bariadi Mji kwa lengo la kutathmini sheria na kanuni za utekelezaji wa majukumu.
Sauti ya Aron Misanga
Aidha Misangu amesema kuwa katika Programu ya Takukuru Rafiki wamefanikiwa kuongeza wigo wa ushiriki katika mapambano dhidi ya rushwa kwa kuibua kero katika jamii zao na kuziwekea mikakati ya kuzitatua.
Sauti ya Aron Misanga